Wednesday, December 9, 2015
USIPUNGUKIWE NA IMANI.
Biblia katika kitabu cha Mathayo 17:18 inasema‘ ..Ni kwa
sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana amini
nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali
mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao
utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu . Hii ni
habari ya yule kijana aliyekuwa na pepo bubu na kiziwi, mzazi
wake akamleta kwa wanafunzi wa Yesu wamwombee. Biblia
inatueleza kwamba wanafunzi walijaribu kumtoa yule pepo
wasiweze, wakati huo Yesu alikuwa amepanda Mlimani kwenda
kuomba.
Yesu aliporudi alielezwa kilichotokea, akawakemea wanafunzi
wake na kisha akamuombea yule kijana akapona. Baadaye
wanafunzi wa Yesu wakamuuliza, kwa nini sisi hatukuweza
kumtoa yule pepo. Ndipo Yesu akawajibu akasema ‘Ni kwa
sababu ya upungufu wa imani yenu… Neno upungufu lina ya
isiyo – tosheleza, yaani imani yao ilikuwa ina upungufu na kwa
hiyo wasingeweza kumtoa yule pepo. Jambo ninalotaka
tuliangalie ni kwamba kwa kuwa tatizo lilikuwa ni upungufu wa
imani yao, ina maana walitakiwa kuongeza imani yao wakati
wanaendelea kukemea. Sasa swali muhimu ni je
wangeongezaje imani yao wakati wako kwenye jaribu/vitani?.
Naam licha ya swali hili kuna maswali mengine ambayo ni
muhimu kuyatafakari ili tuweze kuwa na ufahamu mzuri wa
imani. Je upungufu huu wa imani kwa wanafunzi walikuwa nao
kabla hawajaanza kukemea yule pepo au ulikuja wakati
wanaendelea kuomba. Naam Yesu anatuonyesha kwamba kosa
la hawa wandugu wenzetu lilikuwa upungufu wa imani yao?
Biblia katika Waebrania 11:1 inaeleza kwamba ‘imani ni kuwa na
uhakika wa mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo
yasiyoonekana’ . Kwa hiyo endapo Yesu alisema ni kwa sababu
ya upungufu wa imani yao ina maana ndani yao walipungukiwa
uhakika wa kile walichokitarajia, ambacho ni kufunguliwa/
kuponywa kwa kijana mwenye pepo. Naam upungufu wao wa
imani ulitokana na mashaka juu ya uhakika wa yule kijana
kufunguliwa.
Nini kilipelekea wao kuingiza hofu/mashaka?
Kukosekana kwa dalili za kijana kufunguliwa – Ni imani
yangu kwamba wanafunzi walipoanza kukemea walikuwa
na uhakika kwamba Yule kijana atafunguliwa. Naam kadri
walivyoendelea kuomba na kuona kwamba hakuna
mabadiliko ya aina yoyote kwa mgonjwa yule ndipo hofu/
mashaka yakawaingia mioyoni mwao.
Maneno ya kusikia – Ikumbukwe kwamba chanzo cha
imani yoyote ni kusikia (Warumi 10:17)? Kumbuka wakati
wanendelea kuomba kulikuwa kuna kundi kubwa la watu
ambao walikuwa wanamsubiri Yesu pamoja nao. Hivyo
huenda wakati wanafunzi wanaaendelea kuomba walisikia
watu wakisema, wanafunzi wa Yohana wenyewe
walishindwa kumuombea, wao wataweza, wamejaribu
watumishi wa kila aina wameshindwa, huyu hawezekani
anasubiri kifo, naam haya yote yakapunguza uhakika
ndani yao kwamba kwa jina la Yesu yule kijana anaweza
kupona.
Maneno yao wenyewe – Biblia haituelezi namna/approach
waliyoitumia kuomba/kukemea. Huenda walianza kuomba
mmoja mmoja/ au waliomba wachache na mwishowe
ndipo wakaomba kama kundi. Kwenye kundi lolote kuna
mengi, huenda walipokemea kwa muda kadhaa na bila
kijana kuonyesha dalili za kupona baadhi ya wanafunzi
wakaingiwa na hofu na wakawaambukiza na wengine na
hivyo kushindwa kumtoa pepo. Hebu jaribu kufikiri mtu
kama Yuda Iskariote alikuwa anafanya nini wakati
wenzake wanakemea?
Nini cha kufanya?
Hofu/mashaka ni silaha kubwa sana ambayo Shetani huitumia
kuwafanya watu washindwe kupata majibu ya maombi/miujiza
yao kutoka kwa Mungu . Shetani anafahamu kwamba
imeandikwa ‘Mwenye haki wangu ataishi kwa imani, naye
akisstasita roho yangu haina furaha naye’ (Wabrania 10:38).
Hivyo ili kuharibu/kuondoa imani ya mtu kwa Mungu, silaha
anayotumia ni kuingiza mashaka moyoni mwake dhidi ya ahadi
za Mungu/neno la Mungu kwenye maisha yake. Yesu
aliwaambia hivi wanafunzi wake ‘… amini nawaambia yeyote
atakayeuambia mlima huu ng’oka ukatupwe baharini, wala
asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo
asemayo yametukia, yatakuwa yake’ (Marko 11:22).
Mpenzi msomaji kamwe usimruhusu Shetani kwa kutumia silaha
hii ya mashaka azuie baraka zako na wale wanaokuhusu
maishani mwako. Haijalishi jaribu limesimama mbele yako kwa
kiwango gani usiondoe imani yako juu ya kile ambacho Yesu
amekisema kwenye neno lake juu yako. Naam Mungu wetu si
mtu hata aseme uongo, ahadi zake ni amina na kweli. Naam
katikati ya jaribu/changamoto wewe ongeza imani yako kwa
kupambana na roho ya mashaka/hofu, naam tumia Biblia ili
ikuongoze kukupa mistari ambayo itakuongezea uhakika wa
kufanikiwa katika lile ulifanyalo.
Zaidi kuwa makini na maneno ya kusikia kwa habari ya imani
yako. Wanafunzi wa Yesu walipaswa kutokujali maneno ya
kusikia kutoka kwa watu, au kwa wenzao walioingia mashaka,
naam walipswa kudumu kuamini kwamba kijana atapona naam
ingekuwa hivyo. Je si unakumbuka habari za Petro
alivyoambiwa na Yesu atembee juu ya maji. Awali alianza vema
na akatembea hatua kadhaa juu ya maji. Biblia inasema
dhoruba ilipompiga akaona shaka na kuanza kuzama. Kwa nini
alizama? si kwa sababu Yesu hakuwepo, bali ni kwa sababu
aliona shaka.
Naam kitu kilichopungua kwenye imani ya wanafunzi, ni uhakika
kwamba yule kijana atapona. Na kilichopelekea upungufu wao
wa imani, si kutokumwamini/kumjua Yesu, bali ni kuruhusu
hofu ichukue nafasi ya imani/uhakika waliokuwa nao kwamba
yule mgonjwa atapona. Naam kwa mara nyingine tena
‘usirihusu hofu iharibu muujiza/future yako’ .
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nawe daima.
Tuesday, December 8, 2015
SISI JE! TUTAPATAJE KUPONA? TUSIPOJALI WOKOVU MKUBWA NAMNA HII
Kisha NIKAONA KITI CHA ENZI, KIKUBWA, CHEUPE, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
NIKAWAONA WAFU, WAKUBWA KWA WADOGO, wamesimama mbele ya hicho kiti cha
enzi; na VITABU VIKAFUNGULIWA; na KITABU KINGINE KIKAFUNGULIWA, AMBACHO
NI CHA UZIMA; na hao WAFU WAKAHUKUMIWA KATIKA MAMBO HAYO YALIYOANDIKWA
KATIKA VILE VITABU, sawasawa na matendo yao.
Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. WAKAHUKUMIWA KILA MTU KWA KADIRI YA MATENDO YAKE.
NA IWAPO MTU YE YOTE HAKUONEKANA AMEANDIKWA KATIKA KITABU CHA UZIMA, ALITUPWA KATIKA LILE ZIWA LA MOTO.
(Ufunuo 20:10-15)
Sisi je! Tutapataje kupona, TUSIPOJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia; (Waebrania 2:3)
Ndugu yangu na Rafiki yangu Maandiko yanasema;
Hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana HAPANA JINA JINGINE chini ya mbingu WALILOPEWA WANADAMU LITUPASALO SISI KUOKOLEWA KWALO. (Matendo 4:12)
Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; UZIMA HUU UMO KATIKA MWANAWE. (1Yohana 5:11)
Sasa Unaniuliza, yanipasa nifanye nini ili nipate kuokoka?
Jawabu langu ni hili;
MWAMINI BWANA YESU, NAWE UTAOKOKA PAMOJA NA NYUMBA YAKO. (Matendo 16:31)
Kwani yeye mwenyewe anasema;
Amin, amin, nawaambia, YEYE ALISIKIAYE NENO LANGU NA KUMWAMINI YEYE ALIYENIPELEKA YUNA UZIMA WA MILELE; wala HAINGII HUKUMUNI, bali AMEPITA KUTOKA MAUTINI KUINGIA UZIMANI. (Yohana 5:24)
Kuna leo kuna Kesho, Hakuna ajuaye, Amua mustakabali wa maisha ya baadaye ya kwa kutubu dhambi zako zote na uovu wako wote mbele za MUNGU na Amua kumwamini na kumpokea YESU KRISTO kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yako!
Kumbuka;
Wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; (Yohana 1:12)
Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. WAKAHUKUMIWA KILA MTU KWA KADIRI YA MATENDO YAKE.
![]() |
Na Mchungaji Isaya |
(Ufunuo 20:10-15)
Sisi je! Tutapataje kupona, TUSIPOJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia; (Waebrania 2:3)
Ndugu yangu na Rafiki yangu Maandiko yanasema;
Hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana HAPANA JINA JINGINE chini ya mbingu WALILOPEWA WANADAMU LITUPASALO SISI KUOKOLEWA KWALO. (Matendo 4:12)
Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; UZIMA HUU UMO KATIKA MWANAWE. (1Yohana 5:11)
Sasa Unaniuliza, yanipasa nifanye nini ili nipate kuokoka?
Jawabu langu ni hili;
MWAMINI BWANA YESU, NAWE UTAOKOKA PAMOJA NA NYUMBA YAKO. (Matendo 16:31)
Kwani yeye mwenyewe anasema;
Amin, amin, nawaambia, YEYE ALISIKIAYE NENO LANGU NA KUMWAMINI YEYE ALIYENIPELEKA YUNA UZIMA WA MILELE; wala HAINGII HUKUMUNI, bali AMEPITA KUTOKA MAUTINI KUINGIA UZIMANI. (Yohana 5:24)
Kuna leo kuna Kesho, Hakuna ajuaye, Amua mustakabali wa maisha ya baadaye ya kwa kutubu dhambi zako zote na uovu wako wote mbele za MUNGU na Amua kumwamini na kumpokea YESU KRISTO kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yako!
Kumbuka;
Wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; (Yohana 1:12)
Subscribe to:
Posts (Atom)