Wednesday, December 9, 2015
USIPUNGUKIWE NA IMANI.
Biblia katika kitabu cha Mathayo 17:18 inasema‘ ..Ni kwa
sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana amini
nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali
mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao
utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu . Hii ni
habari ya yule kijana aliyekuwa na pepo bubu na kiziwi, mzazi
wake akamleta kwa wanafunzi wa Yesu wamwombee. Biblia
inatueleza kwamba wanafunzi walijaribu kumtoa yule pepo
wasiweze, wakati huo Yesu alikuwa amepanda Mlimani kwenda
kuomba.
Yesu aliporudi alielezwa kilichotokea, akawakemea wanafunzi
wake na kisha akamuombea yule kijana akapona. Baadaye
wanafunzi wa Yesu wakamuuliza, kwa nini sisi hatukuweza
kumtoa yule pepo. Ndipo Yesu akawajibu akasema ‘Ni kwa
sababu ya upungufu wa imani yenu… Neno upungufu lina ya
isiyo – tosheleza, yaani imani yao ilikuwa ina upungufu na kwa
hiyo wasingeweza kumtoa yule pepo. Jambo ninalotaka
tuliangalie ni kwamba kwa kuwa tatizo lilikuwa ni upungufu wa
imani yao, ina maana walitakiwa kuongeza imani yao wakati
wanaendelea kukemea. Sasa swali muhimu ni je
wangeongezaje imani yao wakati wako kwenye jaribu/vitani?.
Naam licha ya swali hili kuna maswali mengine ambayo ni
muhimu kuyatafakari ili tuweze kuwa na ufahamu mzuri wa
imani. Je upungufu huu wa imani kwa wanafunzi walikuwa nao
kabla hawajaanza kukemea yule pepo au ulikuja wakati
wanaendelea kuomba. Naam Yesu anatuonyesha kwamba kosa
la hawa wandugu wenzetu lilikuwa upungufu wa imani yao?
Biblia katika Waebrania 11:1 inaeleza kwamba ‘imani ni kuwa na
uhakika wa mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo
yasiyoonekana’ . Kwa hiyo endapo Yesu alisema ni kwa sababu
ya upungufu wa imani yao ina maana ndani yao walipungukiwa
uhakika wa kile walichokitarajia, ambacho ni kufunguliwa/
kuponywa kwa kijana mwenye pepo. Naam upungufu wao wa
imani ulitokana na mashaka juu ya uhakika wa yule kijana
kufunguliwa.
Nini kilipelekea wao kuingiza hofu/mashaka?
Kukosekana kwa dalili za kijana kufunguliwa – Ni imani
yangu kwamba wanafunzi walipoanza kukemea walikuwa
na uhakika kwamba Yule kijana atafunguliwa. Naam kadri
walivyoendelea kuomba na kuona kwamba hakuna
mabadiliko ya aina yoyote kwa mgonjwa yule ndipo hofu/
mashaka yakawaingia mioyoni mwao.
Maneno ya kusikia – Ikumbukwe kwamba chanzo cha
imani yoyote ni kusikia (Warumi 10:17)? Kumbuka wakati
wanendelea kuomba kulikuwa kuna kundi kubwa la watu
ambao walikuwa wanamsubiri Yesu pamoja nao. Hivyo
huenda wakati wanafunzi wanaaendelea kuomba walisikia
watu wakisema, wanafunzi wa Yohana wenyewe
walishindwa kumuombea, wao wataweza, wamejaribu
watumishi wa kila aina wameshindwa, huyu hawezekani
anasubiri kifo, naam haya yote yakapunguza uhakika
ndani yao kwamba kwa jina la Yesu yule kijana anaweza
kupona.
Maneno yao wenyewe – Biblia haituelezi namna/approach
waliyoitumia kuomba/kukemea. Huenda walianza kuomba
mmoja mmoja/ au waliomba wachache na mwishowe
ndipo wakaomba kama kundi. Kwenye kundi lolote kuna
mengi, huenda walipokemea kwa muda kadhaa na bila
kijana kuonyesha dalili za kupona baadhi ya wanafunzi
wakaingiwa na hofu na wakawaambukiza na wengine na
hivyo kushindwa kumtoa pepo. Hebu jaribu kufikiri mtu
kama Yuda Iskariote alikuwa anafanya nini wakati
wenzake wanakemea?
Nini cha kufanya?
Hofu/mashaka ni silaha kubwa sana ambayo Shetani huitumia
kuwafanya watu washindwe kupata majibu ya maombi/miujiza
yao kutoka kwa Mungu . Shetani anafahamu kwamba
imeandikwa ‘Mwenye haki wangu ataishi kwa imani, naye
akisstasita roho yangu haina furaha naye’ (Wabrania 10:38).
Hivyo ili kuharibu/kuondoa imani ya mtu kwa Mungu, silaha
anayotumia ni kuingiza mashaka moyoni mwake dhidi ya ahadi
za Mungu/neno la Mungu kwenye maisha yake. Yesu
aliwaambia hivi wanafunzi wake ‘… amini nawaambia yeyote
atakayeuambia mlima huu ng’oka ukatupwe baharini, wala
asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo
asemayo yametukia, yatakuwa yake’ (Marko 11:22).
Mpenzi msomaji kamwe usimruhusu Shetani kwa kutumia silaha
hii ya mashaka azuie baraka zako na wale wanaokuhusu
maishani mwako. Haijalishi jaribu limesimama mbele yako kwa
kiwango gani usiondoe imani yako juu ya kile ambacho Yesu
amekisema kwenye neno lake juu yako. Naam Mungu wetu si
mtu hata aseme uongo, ahadi zake ni amina na kweli. Naam
katikati ya jaribu/changamoto wewe ongeza imani yako kwa
kupambana na roho ya mashaka/hofu, naam tumia Biblia ili
ikuongoze kukupa mistari ambayo itakuongezea uhakika wa
kufanikiwa katika lile ulifanyalo.
Zaidi kuwa makini na maneno ya kusikia kwa habari ya imani
yako. Wanafunzi wa Yesu walipaswa kutokujali maneno ya
kusikia kutoka kwa watu, au kwa wenzao walioingia mashaka,
naam walipswa kudumu kuamini kwamba kijana atapona naam
ingekuwa hivyo. Je si unakumbuka habari za Petro
alivyoambiwa na Yesu atembee juu ya maji. Awali alianza vema
na akatembea hatua kadhaa juu ya maji. Biblia inasema
dhoruba ilipompiga akaona shaka na kuanza kuzama. Kwa nini
alizama? si kwa sababu Yesu hakuwepo, bali ni kwa sababu
aliona shaka.
Naam kitu kilichopungua kwenye imani ya wanafunzi, ni uhakika
kwamba yule kijana atapona. Na kilichopelekea upungufu wao
wa imani, si kutokumwamini/kumjua Yesu, bali ni kuruhusu
hofu ichukue nafasi ya imani/uhakika waliokuwa nao kwamba
yule mgonjwa atapona. Naam kwa mara nyingine tena
‘usirihusu hofu iharibu muujiza/future yako’ .
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nawe daima.
Tuesday, December 8, 2015
SISI JE! TUTAPATAJE KUPONA? TUSIPOJALI WOKOVU MKUBWA NAMNA HII
Kisha NIKAONA KITI CHA ENZI, KIKUBWA, CHEUPE, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
NIKAWAONA WAFU, WAKUBWA KWA WADOGO, wamesimama mbele ya hicho kiti cha
enzi; na VITABU VIKAFUNGULIWA; na KITABU KINGINE KIKAFUNGULIWA, AMBACHO
NI CHA UZIMA; na hao WAFU WAKAHUKUMIWA KATIKA MAMBO HAYO YALIYOANDIKWA
KATIKA VILE VITABU, sawasawa na matendo yao.
Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. WAKAHUKUMIWA KILA MTU KWA KADIRI YA MATENDO YAKE.
NA IWAPO MTU YE YOTE HAKUONEKANA AMEANDIKWA KATIKA KITABU CHA UZIMA, ALITUPWA KATIKA LILE ZIWA LA MOTO.
(Ufunuo 20:10-15)
Sisi je! Tutapataje kupona, TUSIPOJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia; (Waebrania 2:3)
Ndugu yangu na Rafiki yangu Maandiko yanasema;
Hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana HAPANA JINA JINGINE chini ya mbingu WALILOPEWA WANADAMU LITUPASALO SISI KUOKOLEWA KWALO. (Matendo 4:12)
Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; UZIMA HUU UMO KATIKA MWANAWE. (1Yohana 5:11)
Sasa Unaniuliza, yanipasa nifanye nini ili nipate kuokoka?
Jawabu langu ni hili;
MWAMINI BWANA YESU, NAWE UTAOKOKA PAMOJA NA NYUMBA YAKO. (Matendo 16:31)
Kwani yeye mwenyewe anasema;
Amin, amin, nawaambia, YEYE ALISIKIAYE NENO LANGU NA KUMWAMINI YEYE ALIYENIPELEKA YUNA UZIMA WA MILELE; wala HAINGII HUKUMUNI, bali AMEPITA KUTOKA MAUTINI KUINGIA UZIMANI. (Yohana 5:24)
Kuna leo kuna Kesho, Hakuna ajuaye, Amua mustakabali wa maisha ya baadaye ya kwa kutubu dhambi zako zote na uovu wako wote mbele za MUNGU na Amua kumwamini na kumpokea YESU KRISTO kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yako!
Kumbuka;
Wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; (Yohana 1:12)
Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. WAKAHUKUMIWA KILA MTU KWA KADIRI YA MATENDO YAKE.
![]() |
Na Mchungaji Isaya |
(Ufunuo 20:10-15)
Sisi je! Tutapataje kupona, TUSIPOJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia; (Waebrania 2:3)
Ndugu yangu na Rafiki yangu Maandiko yanasema;
Hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana HAPANA JINA JINGINE chini ya mbingu WALILOPEWA WANADAMU LITUPASALO SISI KUOKOLEWA KWALO. (Matendo 4:12)
Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; UZIMA HUU UMO KATIKA MWANAWE. (1Yohana 5:11)
Sasa Unaniuliza, yanipasa nifanye nini ili nipate kuokoka?
Jawabu langu ni hili;
MWAMINI BWANA YESU, NAWE UTAOKOKA PAMOJA NA NYUMBA YAKO. (Matendo 16:31)
Kwani yeye mwenyewe anasema;
Amin, amin, nawaambia, YEYE ALISIKIAYE NENO LANGU NA KUMWAMINI YEYE ALIYENIPELEKA YUNA UZIMA WA MILELE; wala HAINGII HUKUMUNI, bali AMEPITA KUTOKA MAUTINI KUINGIA UZIMANI. (Yohana 5:24)
Kuna leo kuna Kesho, Hakuna ajuaye, Amua mustakabali wa maisha ya baadaye ya kwa kutubu dhambi zako zote na uovu wako wote mbele za MUNGU na Amua kumwamini na kumpokea YESU KRISTO kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yako!
Kumbuka;
Wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; (Yohana 1:12)
IPO NGUVU NDANI YA JINA LA YESU.
![]() |
Na Mchungaji Issaya. |
BWANA YESU ASIFIWE !
Unaweza kuteseka sana hata kama umeokoka kwakutojua nguvu iliyoko ndani ya jina la Yesu inavyo weza kukusaidia
Mungu anasema katika Zekaria 10 :12 : ‘Nami nitawatia nguvu katika BWANA,nao watatembea huku na huko katika Jina lake asema BWANA’
Ndugu mtu wa Mungu,Napenda kwanza ufahamu kwamba Jina la YESU lilikuwa Jina la Mungu wetu akamrithisha YESU,
najua unashangaa ila embu soma Ebrania 1 :4 :’Amefanyika bora kupita malaika,kwa kadiri ya Jina alilorithi lilivyo tukufu kuliko lao.’Kwa hiyo huo mstari wa Zekaria 10 :12 Mungu anasema kuwa atatutia nguvu katika Jina la YESU.
JINA LIPITALO MAJINA YOTE :
Ndugu katika Kristo,Jina la YESU ni Jina linalopita majina yote hapa duniani,kule mbinguni(Ebrania 1 :4) na hata kule kuzimu.Kama Biblia inavyosema Wafilipi 2 :9 : ‘Mungu alimwadhimisha mno,akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina’
Jina la YESU linaokoa,linatubariki,linatuunganisha na Mungu n.k.
NGUVU ILIYOMO KWENYE JINA LA YESU:
NGUVU YA KUFANYA YOTE.
Ndugu,ukweli ni kwamba Jina la YESU linayo nguvu ya kumsaidia kila mtu kufanya kila jambo analotaka kulifanya hapa duniani,mradi tuu iwe ni jambo jema la kumpendeza Mungu.Iwe ni kusoma,kuhubiri kuimba au lolote lile. Angalia Neno la Mungu linavyosema katika Wakolosai 3 :17 : ‘Kila mfanyalo kwa neno au kwa tendo,fanyeni yote kwa Jina la YESU
NGUVU YA KUHUBIRI INJILI YA MUNGU.
Watumishi wote wa Mungu wanapaswa kufahamu kuwa Jina la YESU lina nguvu ambayo itatuwezesha kwenda huku na huko katika kutangaza Injili ya Mungu wetu,kwa maana ni lazima tumuombe Mungu ili atupe nguvu zake.Kumbuka mstari tuliousoma hapo juu wa Zekaria 10 :12.
NGUVU YA KUTULINDA SISI SOTE.
Jina la YESU pia lina nguvu za ajabu sana,na linaweza kabisa kutulinda dhidi ya mapepo,wachawi,majambazi,wezi,ajali na kila hatari iliyopo hapa duniani.Angalia pia Biblia inachosema katika kitabu cha Yohana 17 :11 : ‘.......uwalinde kwa NGUVU YA JINA L AKO ULILONIPA(Jina la YESU).Hayo ni maombi ya YESU akiwaombea wanafunzi wake kwa Mungu,anamwomba awalinde kwa nguvu iliyo kwenye jina la YESU.Tunachotakiwa ni kumwomba Mungu atulinde kwa nguvu iliyo kwenye jina la YESU.
UPONYAJI NA UKOMBOZI
Bwana YESU alisema ‘Kwa kutumia Jina langu watatoa pepo,watasema kwa lugha mpya,watashika nyoka,hata wakinywa kitu cha kufisha hakitawadhuru kabisa,wataweka mikono yao juu ya wagonjwa nao watapata afya’Ndugu napenda ufahamu kuwa Jina la YESU lina nguvu inayotuwezesha kumtumikia Mungu kwa kulitumia jina hilo na kazi ya Mungu ikafanyika.Ni muhimu basi kuomba nguvu ya Jina la YESU kabla ya kwenda kuombea wagonjwa au kukemea pepo au kufanya huduma ya ukombozi au huduma yoyote ile.
LINAMLETA YESU PALE TULIPO.
YESU mwenyewe alisema katika Matayo 18 :20 : ‘Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa Jina langu,nami nipo papo hapo katikati yao’Hii ina maana kuwa popote pale tunapokusanyika halafu tukalitaja Jina la YESU,yeye mwenyewe YESU anashuka na kuwa pamoja nasi hata kama hatumwoni kwa macho yetu.Basi hii ni nguvu nyingine ambayo Mungu ameiweka kwenye Jina la YESU.
NGUVU ZA KIVITA :
Watu wengi hawategemei kuwa Jina la YESU lina nguvu ya kutusaidia katika vita tulivyonavyo hapa duniani.Ni rahisi kwao kuamini kuwa Jina hili lina nguvu kutushindia vita vya kiroho lakini si vya majeshi ya wanadamu.Kama umeingia vitani kwa kibali cha Mungu,basi Jina la YESU lina uwezo wa kukusaidia ushinde hivyo vita.Mkumbuke Mfalme Daudi wakati alipomwua Goliathi kwa kombeo la jiwe,hebu tusome Biblia 1Samweli 17 :45 : ‘Daudi akamwambia....lakini mimi nakujia kwa Jina la BWANA(Jina la YESU) wa majeshi,Mungu wa majeshi ya Israeli..’Ni wazi kuwa yule Goliathi alikuwa amejiandaa kuingia vitani hii ikiwa ni pamoja na kuvaa mavazi ya kuulinda mwili wake,na kwasababu hiyo ilikuwa si rahisi kwa nguvu za kibinadamu kumuua Golithi kwa jiwe la kombeo,lakini yeye Daudi hakuingia vitani kwa nguvu zake bali aliingia kwa nguvu za Jina la YESU,alipoingia vitani kwa Jina hilo,YESU aliteremsha msaada na nguvu zake kwa Daudi ndio maana akamwua Goliathi kwa jiwe la kombeo.Soma pia Zaburi 44 :5b,na Zaburi 20 :7 : ‘Hawa wanataja magari,hawa farasi lakini mimi nitalitaja Jina la Bwana Mungu wangu(Jina la YESU)’
KUAMURU UNACHOTAKA KITOKEE KUTOKEA.
Kwa kutumia jina la YESU tunaweza kuamuru chochote ambacho ni chema mbele za Mungu kitokee kikatokea kweli.
ITUMIE HIYO NGUVU
Natumaini kuwa umejifunza na kufahamu baadhi ya nguvu zilizomo kwenye Jina hili la ajabu,Jina la YESU Kristo.Sasa unachotakiwa kufanya ni wewe kuitumia hiyo nguvu iliyopo kwenye Jina hilo.
Ili uweze kulitumia Jina la YESU ni muhimu kumuomba Mungu mambo yafuatayo :
UHALALI WA KULITUMIA :
Ili kulitumia Jina la YESU ni lazima Mungu akupe uhalali wa kulitumia Jina hilo.Kumbuka kilichowapata watoto wa mtu mmoja aliyeitwa Skewa(Matendo 18 :11-16),vijana hawa walitaka kulitumia Jina la YESU kukemea pepo huku hawajaokoka,matokeo yake yule pepo akawadhuru.Kupata uhalaliwa Kulitumia Jina la YESU ni lazima KUOKOKA kwanza kama hujaokoka.
IMANI JUU YA JINA HILO :
Ili kulitumia Jina la YESU ni lazima kwanza uwe na imani juu ya Jina hilo,uliamini kuwa linaweza YOTE.Kama Biblia isemavyo kuwa kuwa Imani huja kwa kusikia Neno la Kristo(Warumi 10 :17)basi ni lazima kusoma maandiko sahihi yanayofundisha kuhusu Jina la YESU.
MAMLAKA YA KULITUMIA :
Ukishaokoka unakuwa na uhalali wa kulitumia Jina la YESU lakini si mamlaka,hivyo ni lazima kumwomba Mungu akupe mamlaka ya kulitumia Jina hilo.
UPAKO WA KULITUMIA :
Unahitaji pia upako kutoka kwa Mungu wa kukusaidia na kukufundisha kulitumia Jina la YESU katika maisha yako,mwombe Mungu akupe upako huo.
MBINU ZA KULITUMIA :
Huwezi kulitumia Jina la YESU bila kujua mbinu za kulitumia,hivyo mwombe Mungu akupe mbinu za kulitumia Jina hilo,naye atakufundisha.
Natumaini kuwa somo hilo limekusaidia sana,tafadhali nifahamishe namna somo hili lilivyokusaidia.
UKOMBOZI WAKO UNAPATIKANA KWA MAAMUZI YAKO MWENYEWE.
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
MUNGU ameachilia vitu fulani ambavyo kama tukivishika vitatuvusha na kutupeleka sehemu nyingine nzuri.
Ndugu mmoja kabila mmasai aliambiwa ajitetee mahakamani, akakimbia baada ya kuambiwa ajitetee, na watu wa mahakama wakashindwa kumkimbiza maana badala ya kumkimbiza wakabaki wakicheka tu, lakini hiyo ndio ikawa pona yake yule ndugu mmasai. Yeye aliambiwa ajitetee kwa maneno yake yeye akajitetea kwa miguu yake lakini akapona maana alijitetea.
Warumi 10:9-11 ''Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika.''
Neno la MUNGU linatupa jinsi ambavyo tunaweza kuokolewa na kuupata uzima wa milele bure, Lakini watu wa MUNGU wengi wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.
Hosea 4:6 ''Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya MUNGU wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.''
Binadamu wengi sana wanadhani hadi Malaika awahubiri ndipo wataona umuhimu wa kumpokea BWANA YESU na kujiponya raho zao na Nafsi zao.
Mmasai alipoambiwa ajitetee hakika alijitetea lakini wanadamu wengi leo wakiambiwa wajitetee kwa kuzikimbia dhambi na kumkimbilia YESU watasena '' subiri kwanza, au watasema ''labda mwakani''
Hawana uhakika wa kuishi hiyo mwakani lakini hiyo mwakani ndio wameipangia mipango mingi kuliko leo yao.
=MUNGU amewasogezea karibu kabisa wanadamu uzima wa milele lakini kwa kukosa kwao maarifa wameukataa Wokovu wa MUNGU.
=MUNGU amewasogezea uzima wa milele karibu yao sana tena amewasogezea kwenye vinywa vyao kabisa lakini bado wanadamu kwa kukosa kwao maarifa ya MUNGU wameukataa Wokovu wa BWANA YESU ambao ni wa thamani kwao kuliko yote wanayoyahitaji maishani mwao.
=Wengine kwa kukosa maarifa wameshika madhehebu yao huku YESU yuko pembeni wamemwacha.
=Wengine kwa kukosa maarifa wanafuata dini za wazazi wao japokuwa ni dini za shetani kabisa.
Neno la MUNGU katika Warumi 10:13 Linasema ''kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la BWANA ataokoka.'' Lakini kwa kukosa maarifa wanadamu wengi wanaukataa Wokovu huo wa BWANA YESU.
Kwa kukosa maarifa wanadamu wengi wanamkataa BWANA YESU mwenye uzima wao wa milele.
-Ukombozi utatokana na wewe mwenyewe.
-Ukombozi utapatikana kwa maamuzi yako Mwenyewe.
-Ukombozi wako uko katika KRISTO YESU pekee lakini wewe utaumiliki ukombozi huo kwa kuufuata huku ukidharau ya dunia na kuacha uovu wote.
Ndugu, Usikubali kuishi na mapepo maishani mwako huku ukijua kabisa kwamba mapepo ni mashetani ambayo yametumwa kwako ili kuhakikisha hufiki mbinguni.
Kataa leo kutumiwa na shetani kama chombo chake cha kumburudisha.
Watu wengi wamefungwa kwenye mambo mengi huku wakijua kabisa kuwa MUNGU anaweza kufanya muujiza katika hayo lakini kwa kukosa maarifa kwao hawamwendei MUNGU kwa maombi hata wakapokea baraka zao hizo.
Japokuwa MUNGU ''Amewapelekea watu wake ukombozi, Ameamuru agano lake liwe la milele, Jina lake ni takatifu la kuogopwa.-Zaburi 111:9'' Lakini wanadamu wengi wameukataa ukombozi wa MUNGU ambao pekee uko katika YESU KRISTO.
Kwa kukosa maarifa wanadamu wako tayari kumchagua shetani na kumkataa YESU.
Kwa kukosa maarifa wanadamu wengi wako tayari kumwabudu shetani hata kama wanajua kabisa kwamba anayestahili kuabudiwa ni MUNGU pekee, tena MUNGU huwa haabudiwi kwa mazoea bali huabudiwa katika ROHO na kweli.
Yohana 4:24 ''MUNGU ni ROHO, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. ''
Wanadamu wengi mimi naona huwa wanapenda zaidi ukumbusho na sio ukombozi wa roho zao.
Wanadamu wako tayari wakifa wakumbukwe kwamba walikuwa walevi wenye uwezo wa kumaliza kreti ya bia moja kwa siku.
Kuna ambao wako tayari wakumbukwe kwamba walikuwa viwembe na walitembea na mabinti/vijana wa mitaa mitatu yote.
Ni kumbukumbu mbaya na ni kumbukumbu ya waliokosa maarifa sahihi ya kiMUNGU.
Ni ukumbusho wataacha kwa sababu ya uovu wao uliopindukia lakini hiyo itawasaidia nini kwa habari ya uzima wa milele?
Bibi mmoja kwenye Biblia jina lake Anna alikuwa anaungojea ukombozi wa KRISTO na akauona na kumtukuza MUNGU.
Bibi huyu licha ya kuwa mjane kwa miaka 84 lakini aliendelea kuomba na kufunga maana ameichagua njia ya uzima.
Ukombozi ulipofika Biblia inasema kwamba Bibi
''Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru MUNGU, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake.-Luka 2:38''
Je, wewe ndugu unayesoma ujumbe huu unataka kuacha historia gani duniani?
Je na wewe uko katika kundi la watakaoacha heshima bar huku wao wakielekea jehanamu?
Je unaacha heshima mtaani kwa kuwa ulikuwa mzinzi grade A.
Itakusaidia nini kupata vitu vyote vya duniani kisha ukapata hasara ya milele.
Nakushauri leo okoka na anza kuishi maisha matatifu.
Uzima wa milele upo na jehanamu ipo pia lakini ashukuriwe MUNGU kwa kutuletea ukombozi wa roho zetu ambao uko katika KRISTO YESU pekee.
Ndugu ukombozi wako unapatikana kwa maamuzi yako mwenyewe leo ya kumpokea YESU KRISTO.
Yeye BWANA YESU anasema ''Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. -Mathayo 11:28''
Amua vyema leo itakusaidia.
Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
VIWANGO VINNE(4) VYA NENO LA MUNGU KWA MKRISTO.
![]() |
na Peter Mabula |
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU la kutuvusha na kutushindia.
Ujumbe huu MUNGU ameuhifadhi ndani yangu kwa mwaka mzima sasa lakini leo amenipa kibali nikuletee.
Kuna viwango vinne vya Neno la MUNGU kwa Mwamini, mkristo aliyeokoka.
Kila Mkristo aliyeokoka yuko katika kiwango kimojawapo kati ya viwango hivi vinne ninavyokuletea.
Kupitia ujumbe huu naomba ujipime umefikia kiwango gani.
Lakini unapojifunza ujumbe huu naomba ujue pia kwamba uwezekano wa kupanda kutoka kiwango kimoja kwenda kingine upo na upo leo kwa ajili yako.
Hivyo baada ya ujumbe huu utatakiwa ukue kiroho na kufikia kiwango cha juu.
Zaburi 12:6 ''Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.''
Neno la MUNGU ni maneno safi na Neno ni jipya kila siku.
Unajua Neno la MUNGU kwa nini ni jipya kila siku?
Ni kwa sababu Neno kila siku ni kama Pesa mpya inayoanza kutumika.
Wakati Serikali inapotoa Noti mpya naamini kila mtu anatamani kuwa na noti mpya na sio zile za zamani. sasa Neno kila siku ni jipya na Biblia imesema hapo juu kwamba Neno la MUNGU ni kama pesa mpya iliyojaribiwa kalibuni tu tena Pesa hiyo imesafishwa mara saba ndipo ikaanza kutumika, ndivyo neno la MUNGU lilivyo siku zote.
=Ukiona umeanza kulichoka Neno la MUNGU tambua kwamba wewe umeanza pia kuichoka mbingu.
=Kupitia Neno la MUNGU tunamjua MUNGU na mpango wake kwetu.
=Kupitia Neno la MUNGU kila mtu anajua ameandaliwa kitu gani baada ya kuondoka duniani.
VIWANGO VINNE VYA NENO LA MUNGU KWA MWAMINI NI;
1. Kiwango cha maziwa.
Kiwango cha maziwa ni kiwango cha neno la MUNGU ambaco mtu anakipokea baada tu ya kumpokea YESU kama BWANA na MWOKOZI wake.

Mama anapozaa mtoto humwesha maziwa tu kwa miezi 6 maana mtoto huyo kwa muda huo anakuwa hawezi kukipokea chakula kingine.
Kiroho mtu anapookoka maana yake amezaliwa upya kiroho.
amezaliwa na MUNGU kiroho na anaanza kuitwa mtoto wa MUNGU(Yohana 1:12-13).
Mtu anapozaliwa kiroho anakuwa ni kama mtoto mchanga kiroho maana mambo mengi anakuwa hajayajua bado. Huyu anahitaji kunywa maziwa maana chakula bado anakuwa hakiwezi.
Lakini kuwa kanisani miaka 5 au 20 au 30 haiwezi kukufanya kuvuka kiwango cha maziwa kama hukui kiroho.
=Kukua kiroho huwa ni juhudi binafsi za Mwamini.
Mtu ambaye yuko katika kiwango cha maziwa anatakiwa awe na wasimamizi wazuri wa kumsaidia na kumwendeleza kukua kiroho.
Maziwa ni matamu na rahisi kunywa.
Ndio maana kuna baadhi ya makanisa wana madarasa ya kuukulia wokovu ambapo madarasa hayo yanakuwa na walimu wanaowafundisha waamini wapya mafundisho ya kuukulia wokovu.
Mtu wa kiwango cha maziwa chakula kigumu anakuwa bado hakiwezi.
=Kiwango hiki huambatana na imani haba kwa baadhi ya watu.
Mfano;
Kama mchungaji atatangaza maombi ya siku 21 ya kufunga mara zote watakaolalamika au hata kuhama kanisa ni wale wa kiwango cha maziwa, hata kama watu hao wana miaka 12 kwenye wokovu.
Mtu wa kiwango cha maziwa ni rahisi shetani kumdanganya maana huyu ndugu anakuwa hajui mambo mengi ya MUNGU.
Mwenye kiwango cha maziwa ni mtoto kiroho au ni mchanga kiroho.
Mtu kama huyo huwezi kumfundisha mambo magumu maana yanaweza kumkimbiza kanisani kabisa japokuwa hayo magumu ndio muhimu zaidi kwake.
Kama wachungaji wangekuwa wanatangaza kila wiki kile watakachofundisha wiki inayofuata hakika wenye kiwango cha maziwa wangepata taabu sana hata kukimbia kanisa.
Mfano mchungaji atangae kwamba ''Wiki ijayo nafundisha juu ya fungu la kumi maana ni laana kutokutoa fungu la kumi''
Wenye kiwango cha maziwa hata kama wako katika kaisna kwa miaka 2 itawasumbua sana.
Mfano Mchungaji aseme ''Wiki ijayo nitafundisha juu ya kusimama imara kwenye dhoruba kama Stephano, maana Stephano alipigwa mawe hadi kufa lakini alivumilia''
Ujumbe kama huo kwa muumini ambaye yuko kiwango cha maziwa utampa maswali mengi. mfano atawaza kumbe kuna kuuawa, kumbe kuna magumu hivi katika imani hii. hayo atayawaza kwa sababu yeye ni mchanga kiroho na anatakiwa aimalishwe kwanza kwa mafundisho ya kuukulia Wokovu.
=Juhudi ya Mwamini katika maombi, utakatifu, kumtii MUNGU na kujifunza Neno Kanisani ndivyo vitamuondoa haraka kutoka kwenye kiwango cha maziwa hata akahitaji chakula kingine cha kumletea nguvu zaidi mwilini mwake.
Kuna watu hata miezi 3 tu inamtosha kabisa kuhama kutoka kiwango cha maziwa na kuingia kiwango kingine maana kwa muda huo atakuwa kila ibada anahudhuria na kujifunza neno la MUNGU na kulishika na kulitii Neno hilo, atakuwa mwanamaombi na atakuwa akimtumikia MUNGU.
Kuna Wakristo kwa sababu ya kupuuzia kile wanachofundishwa kanisani wamebaki kwenye kiwango cha maziwa tu miaka yote.
Ni watoto wachanga kiroho hata yakija magumu kidogo tu kanisani watakimbia maana ni wachanga kiroho.
Siku moja kuna ndugu mmoja kutoka dini nyingine nje na Ukristo. Yule ndugu alipookoka tu aliniuliza nimwambie YESU ni nani?
Kwa sababu ameokoka muda huo huo nilimwambia kwamba Biblia inasema katika Yohana 3:31 kwamba aliyetoka mbinguni yaani BWANA YESU yu juu ya yote, hivyo YESU anaokoa na kuponya.
Ndugu huyu alifurahi na kusema hakika imani yenu Wakristo ni ya kweli. Baada ya kuukulia wokovu na kulijua Neno vizuri na kukionja kipawa cha ROHO, ndugu huyu haikumsumbua kujua kwamba YESU ni Mwana wa MUNGU, Haikumsumbua kujua kwamba ina maana gani kusemwa kwamba YESU ni Mwana wa MUNGU, Haikumsumbua kusemwa kwamba YESU KRISTO ni MUNGU mkuu(Tito 2:13).
Ndugu huyo hata sasa ni mtumishi mzuri wa MUNGU lakini kama ningempa chakula kigumu siku ya kwanza tangu aachane na dini yake na kuokoka hakika angerudi tu kwenye dini na kukosa uzima wa BWANA YESU.
Watumishi wa MUNGU wanatakiwa kuelewa kiwango cha neno cha wanaowapelekea neno.
2. Kiwango cha Nyama au kiwango cha Chakula cha kawaida.
Yohana 6:27 '' Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa muhuri na BABA, yaani, MUNGU.''
Neno la MUNGU ni chakula cha uzima ila kuna viwango vya chakula hiki kwa mwamini.
Wenye kiwango hili ni wale ambao wamekuwa kidogo kiroho lakini shetani ana uwezo wa kuwayumbisha. Mtu wa kiwango hiki anaweza kuwa anajua mambo mengi kidogo ya ki MUNGU bila kuyatendea kazi.
Waamini wengi sana wako katika kiwango cha nyama.
Mtu kama huyu anaweza akafanya baadhi ya vitu kanisani hata baadhi ya huduma lakini akiambiwa
mfano;wiki ijayo tutakuwa na ibada ya changizo kwa ajili ya kujenga kanisa anaweza asije kanisani siku hiyo na kwenda kuabudu kwingine akidhani anafanya jambo jema kumbe sio.
Mtu kama huyo akiambiwa ijumaa ijayo vijana wote wa kanisani tutatekwenda kwenye mkesha kigamboni anaweza hata akatoa udhuru wa uongo kwa sababu tu hataki kwenda.
=Kiwango hiki huambatana na mazoelea ya ibada.
Mtu wa kundi hili hufanya vitu kwa kujisikia na kusingizia hadi apate amani moyoni ndipo atende jambo hilo la kiMUNGU kumbe ni upungufu wake wa kiwango cha neno ndani yake.
Mtu wa kiwango hiki anaweza hata akachagua vitu vya kushika huku vingine ambavyo ni muhimu akiviaacha.
Mtu kama huyo anakuwa anajua neno kwa sehemu lakini hataki neno limuongoze wala kumuendeza katika njia zake.
Kuna watu wanajua kabisa kwamba viburi ni dhambi lakini wanawafanyia kiburi hata baba zao wa kiroho.
Ingawa anajua kabisa kwamba fungu la kumi ni lazima lakini mtu wa kundi hili anaweza akatoa mwezi huu kisha mwezi ujao akapotezea, ni mbaya na anatakiwa atamani kukua zaidi maana uwezekano wa kuingia kiwango bora zaidi upo wazi kwa kila mwamini.
3. Kiwango cha nyama ngumu au chakula kigumu.
Kiwango hiki ni kiwango cha watu ambao wameshakua kiroho lakini kuna vitu vichache wanavihitaji ili kukamilika ipasavyo.
Mtu wa kundi hili ni ni yule ambaye ameshakuwa kiufahamu wa Neno la MUNGU na ana uelewa wa kutosha.
Mtu huyu anakuwa anafahamu haki zake zote lakini hajaanza kushirikiana na haki zake hizo.
Waebrani 5:12-14 '' Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya MUNGU; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu. Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.''
Mtu wa kundi hili anaweza kuwa anajua mambo mengi sana ya kiMUNGU.
Anaweza akakariri kichwani hata mistari 50 ya Neno la MUNGU lakini hajui jinsi ya kushirikiana na maandiko hayo ili apokee hitaji lake.
Anaweza akajua na kukariri maandiko mengi lakini hajui kutumia Neno hilo ili kufunga na kuharibu nguvu za giza.
Kiwango hiki ni kizuri kiasi lakini mara nyingi watu wa kiwango hiki hawajui maarifa sahihi na jinsi ya kufanya ili kushirikiana na neno la MUNGU hata kuingia katika baraka yao.
=Kiwango hiki wakati mwingine huambatana na kiburi cha uzima na kujiona bora kuliko wengine.
4. Kiwango cha Asali.
Kiwango cha mwisho cha Neno la MUNGU kwa mwamini kinaitwa kiwango cha asali.
Ni kiwango adimu sana na inawezekana kabisa ni wachache walio nacho kiwango hiki.
Kila Mkristo anatakiwa kukifikia kiwango hiki.
=Kiwango hiki huambatana na imani timilifu na utakatifu halisi.
Wa kwanza kutembea katika kiwango hiki ni BWANA YESU mwenyewe alipokuwa duniani.
Isaya 7:14-15 '' Kwa hiyo BWANA mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli. Siagi na asali atakula, wakati ajuapo kuyakataa mabaya na kuyachagua mema. ''
Ukiwa katika viwango vitatu vya kwanza kuna vitu vya kiMUNGU unaweza kuvikosa maana sio saizi yako.
Kiwango hiko cha asali ni kiwango ambacho mhusika anaweza kupokea vitu vikubwa na anaweza kuvumilia katika yote kwa ajili ya BWANA YESU.
Ufunuo 10:9 ''Nikamwendea malaika yule nikamwambia kwamba anipe kile kitabu kidogo. Akaniambia, Kitwae, ukile, nacho kitakutia uchungu tumboni mwako, bali katika kinywa chako kitakuwa kitamu kama asali.''
Katika maono mtume Yohana anakifikia kiwango cha asali na ndio maana alipewa kujua hata mambo ya siku za mwisho hata akatuandikia sisi.
=Kwa kadri unavyokula Neno la MUNGU kwa kujifunza ndivyo unaweza kukua hata kufikia kiwango cha asali.
Mtu wa kiwango hiki hata akiambiwa utakufa wiki hii maana kuna maono yameonekana hivyo yeye ataomba na kumuuliza ROHO MTAKATIFU na ROHO atasema jambo hilo sio kweli na ndugu huyu atasonga mbele maana yuko katika kiwango kikubwa kiimani na kiufahamu wa Neno la MUNGU.
Mfano mtu wa kiwango cha maziwa akiambiwa atakufa wiki hii kwa maono yeye atakimbilia msaada kwa mganga wa kienyeji.
akiambiwa mtu wa kiwango cha nyama anaweza hata kukimbilia polisi kushitaki.
Ni muhimu kupanda na sio kushuka kiviwango.
Ezekieli 3:1-3 '' Akaniambia, Mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kisha enenda ukaseme na wana wa Israeli. Basi nikafunua kinywa changu, naye akanilisha lile gombo. Akaniambia, Mwanadamu, lisha tumbo lako, ulijaze tumbo lako kwa hili gombo nikupalo. Ndipo nikalila, nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu, kama utamu wa asali. ''
Kwa njia ya maono Ezekieli naye anakifikia kiwango hiki.
Asali hakika ni tamu na Neno la MUNGU kwa watu ambao wako kiwango cha asali ni tamu sana kwao jakupua kwa walio viwango vya chini wataona Neno hilo kama chungu na gumu.
=Mtu akiwa katika kiwango hiki anaweza akapewa vitu vingi na MUNGU vya kihuduma na maono pia.
Mithali 24:13-14 ''Mwanangu, ule asali, kwa maana ni njema, Na sega la asali lililo tamu ulionjapo. Basi utaijua hekima kuwa tamu kwa nafsi yako; Ikiwa umekwisha kuiona; Ndipo itakapofuata thawabu; Wala tumaini lako halitabatilika.''
Natamani niendelee lakini kwa leo naishia hapo.
Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
USIUFUATE MWILI BALI OKOKA.
BWANA YESU apewe sifa ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Leo nazungumzia Mwili.
Ndugu Usiufuate Mwili Bali Mtii MUNGU.
Wagalatia 5:16-17 ''Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.''

= Mwili Ni Adui.
=Mwili Una Mawazo Machafu Ambayo Ndio Chanzo Cha Anguko
Kuufuata mwili ni kufuata mambo ya dunia ambayo Biblia inakataza.
2 Kor 10:3-5 '' Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;''
Mawazo Na Fikra Ndio Injini Ya Mwili.
Dhambi Huanzia Akilini Na Kutekemkia Moyoni.
Alivyo Mtu Moyoni Ndivyo Alivyo
Mithali 23:7a ''Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo''
= Ndugu Sulubisha Mwili Wako, Omba.
Kuna watu miili yao imewasababishia wakawa mbali na Wokovu wa MUNGU ambao uko pekee katika BWANA YESU.
Kuna watu hufanya matendo mabaya wakidhani ni sawa tu, huenda kanisani na kudhani ni sawa tu. ni mbaya sana.
Wengine hudhani wana MUNGU lakini huku wakiendeleza mambo ya mwili. Ni mbaya sana.
Japokua watu wengi wanateswa na miili yao lakini jawabu lipo.
jawabu ni YESU KRISTO.
Mimi ngoja nifafanue jinsi ya kuokoka.
Kumpokea YESU KRISTO ni:
1. Kujua wewe ni mwenye dhambi na kumgeukia MUNGU na kutubu.
2. Kumtegemea MUNGU akusamehe.
3.Kumkaribisha YESU KRISTO atawale maisha yako kwa imani ili uwe kama anavyopenda.
Baada ya hayo jina lako litakuwa limeandikwa mbinguni kwenye kitabu cha uzima na pia utakuwa na kinga yaani damu ya YESU KRISTO dhidi ya majini, mapepo na wachawi maana ukiliitia jina la BWANA muda wowote utapona.
Warumi 10:9-10 '' Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.''
Biblia pia iko wazi ikizungumza kwamba nje na KRISTO hakuna uzima wa milele, hivyo kwa yeyote anayeutaka uzima wa milele ni muhimu sana kumpokea YESU.
''Yohana 14:6 ''YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi.''
Ni faida kuu kumpata YESU KRISTO maishani mwako.
Matendo 4:12 ''Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. ''
BWANA YESU mwenyewe anasema juu wanaouhitaji uzima wake wa milele kwamba
'' Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. - Mathayo 11:28''
Kuna faida kubwa kuokoka na kuanza kuishi maisha mataktifu.
Kumpokea YESU na kumtii ni uzima kabisa.
Hakuna uhakika wa uzima popote ila kwa BWANA YESU .
Warumi 8:1''Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika KRISTO YESU.''
Je umempokea YESU?
Kama umempokea YESU unatakiwa uanze kuishi kwa kuongozwa na ROHO wa MUNGU.
Kama umeokoka hakikisha haufuati mwili bali neno la MUNGU.
Wale wanaufuata Neno La MUNGU Biblia inasema hivi juu yao.
Ni heri kuokoka na kuishi maisha matakatifu ili uwe na uhakika wa uzima wa milele.
2 korintho 5:17 '' Mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe kipya tazama ya kale yamepita , na tazama yamekuwa mapya''
Ndugu, Usiufuate Mwili bali okoka na anza kuishi maisha matakatifu.
Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
JE WEWE NI MTU SAHIHI?
Na Mtumishi Peter Mabula |
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Mkristo sahihi akifanya jambo sahihi katika muda sahihi na kwa njia sahihi ni lazima tu atapata matokeo sahihi.
Mkristo halisi ni yule aliyempokea YESU.
Yohana 1:12-13 ''Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake;
waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU''
Hiyo ni A ya Mkristo sahihi lakini B yake ni hii.
'' Umtumaini BWANA ukatende mema, Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.-Zaburi 37:3''
Mkristo halisi humtumaini na kumtegemea BWANA kwa maombi na imani.
Mkristo halisi huishi maisha ya uaminifu kwa MUNGU.
Lakini pia napenda ujue kwamba;
Usahihi wa mtu hauji kwa sababu ya elimu yake bali usahihi unakuja kwa mtu huyo kuongozwa na Neno la MUNGU.
''Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.-Zaburi 119:11''
Ndugu yangu nadhani sasa umekwisha kumjua mtu sahihi.
Je, wewe ni mtu sahihi?
Je, unaoshirikiana nao kila siku ni watu sahihi?
Katika wote unaoshirikiana nao naomba ujue kwamba sio wote ni sahihi na sio wote sio sahihi.
Kuna watu walipompokea YESU hakika walifanyika Wakristo sahihi tena wakristo halisi lakini usahihi wao ulianza kuondolewa na marafiki zao, uharisi wao ulianza kuondolewa na wale wa karibu yao katika maisha.Biblia inatoa ushauri kwa mtu sahihi kuufuata kwamba
''Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.-Zaburi 1:1-2''
Sheria ya BWANA inaitwa Biblia takatifu, hiyo ndio inatakiwa kumpenzeza huyu mtu sahihi kila siku.
Sheria ya BWANA ndio Neno la MUNGU ambalo lipo kutusaidia hivyo kama sisi ni watu sahihi hatutakiwi kuwa mbali na Neno la MUNGU maana kuishi maisha ya kumpendeza MUNGU ni lazima tulifuate na kulitii Neno la MUNGU siku zote.
Japokuwa kuna Wakristo wengi sahihi lakini wameshindwa kuujua muda wao sahihi wa kufanya jambo sahihi ili wapokee kitu sahihi kuoka kwa MUNGU.
Kaina na Habili walikuwa Wacha MUNGU sahihi lakini Habili aliitumia nafasi sahihi katika muda sahihi kufanya jambo sahihi ambalo lilimletea baraka sahihi.
Biblia inasema kwamba
'' Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA. Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake; bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana. BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. -Mwazo 4:3-7''
-Hapa tunajifunza kwamba Habili alifanya jambo sahihi katika muda sahihi hibyo akapokea baraka sahihi kutoka kwa MUNGU.
-Hapa pia tunajifunza kwamba Kaini hakufanya jambo sahihi japokuwa jambo hilo lisilo sahihi alilifanya katika muda sahihi hivyo hakupokea baraka sahihi.
Wakristo wengi wa leo huwa hawafanyi jambo sahihi katika muda sahihi hata wakapokea baraka sahihi.
unaweza ukakuta Binti/Kijana sio sahihi kwa sababu ni mzinzi, lakini licha ya kutokuwa sahihi lakini utakuta anataka kupata baraka sahihi jambo ambalo haliwezekani.
Wengine ni Wakristo sahihi kabisa lakini muda sahihi umefika na ameudharau japokuwa jambo lake ni sahihi hivyo wakati yeye atataka jambo hilo sahihi muda hautakuwa sahihi hivyo atakosa kupata baraka sahihi.
Lakini pia kuna watu sahihi walivumilia katika usahihi wao hata muda sahihi wa baraka yao ukafika hivyo wakapokea baraka sahihi.
Muda sahihi kwa mtu sahihi ukifika hakuna anayeweza kumpinga.
Hesabu 23:8,20 ''Nimlaanije, yeye ambaye MUNGU hakumlaani? Nimshutumuje, yeye ambaye BWANA hakumshutumu? Tazama, nimepewa amri kubariki, Yeye(MUNGU) amebariki, nami siwezi kulitangua.''
Muda sahihi hutolewa na MUNGU na sio mwanadamu.
Muda sahihi ni muda wa mema na sio mabaya.
Muda sahihi hubeba baraka na ushindi.
Changamoto kwa watu wengi huwa hawajui tu muda sahihi ndio maana hubaki vile walivyo.
Mhubiri 3:1,7 '' Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;''
Sio kila muda ni sahihi na ndio maana kuna muda wa kuomba ambao ni tofauti na Muda wa kuacha kuomba maana jambo hilo umejibiwa.
Muda wa jangwani ni tofauti na Muda wa Misri.
Muda wa Kaanani ni tofauti na Muda wa jangwani.
Inawezekana kabisa Jangwani ulikuwa unapewa chakula cha mbinguni(Mana) Lakini kaanani unatakiwa ulime na BWANA atabariki kazi za mikono yako kama ukimtii. Hiyo ndio tofauti ya muda sahihi na pahali sahihi kwa muda huo sahihi uliopo wewe mtu sahihi.
Utu wako ni wa thamani sana na unatakiwa kutunzwa sana.
Hakuna anayeweza kuutunza utu wako ila ni wewe mwenyewe.
Kama hutaweza kuutunza utu wako utakuwa hujui thamani ya utu wako ambayo MUNGU amekupa.
Waefeso 5:3-5 ''Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru. Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa KRISTO na MUNGU.''
Utu wako unatunzwa kwa;
-Wewe kukataa kutumiwa na shetani.
-Unautunza utu wako kwa kutenda yanayompendeza MUNGU tu.
-Unautunza utu wako kwa wewe kutunza Wokovu wako ambao kwa huo utafurahi milele katika uzima wa milele ambao BWANA YESU amekuandalia.
Ukiudharau utu wako hata ukafanya dhambi, hiyo ni kwa hasara yako mwenyewe.
MUNGU anakupenda sana ndio maana uko hai leo kwa neema yake, fanya matendo mema ili uwe rafiki wa MUNGU siku zote.
Kama umeokoka hakika wewe ni mtu sahihi ambaye kwa maombi yako sahihi utapokea baraka sahihi.
Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
ROHO MATAKATIFU KATIKA MAOMBI YAKO NI MUHIMU SANA.
Na Mtumishi Peter Mabula |
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze lakini kabla ya ujumbe leo nataka tuombe.
Tuombe;
''Tunakushukuru MUNGU BABA Kwa Kuwa Wewe U Mwema, Na Kwa Maana Fadhili Zako Ni Za Milele. Ikawa Asubuhi Na Ikawa Jioni Bado Tunaishi Kwa Kulindwa Na Wewe.
U MUNGU Milele Na Utabaki Kuwa MUNGU, Unaitwa NIKO AMBAYE UKO Na Ndio Maana Hata Kufika Leo Umekuwako Ukitulinda.
Hatuna Cha Kukulipa Ambacho Kinalingana Na Upendo Wako. Wakati Maadui Zetu Wakiumiza Vichwa Ili Watudhuru, Malaika Wako BWANA Uliowatuma Wanaumiza Vichwa Kwamba Wawapige Wapi Maadui Zetu.
Tunakushukuru BWANA Kwa Uzima Na Ushindi Uliotupa.
Najua BWANA Wewe Unayajua yangu,
Tena Unasikia Maombi Yetu, Unatazama Neno Lako Na Hakika Unatujibu Maombi Yetu.
Tunapenda Kukuabudu Kila Dakika Maana Wewe Ndio MUNGU. BWANA MUNGU Asante Kwa Silaha Ulizotupa, Umetupa Neno Lako Na ROHO Wako, Umetupa Damu Ya YESU Na Jina La YESU Ndio Ndio Silaha Ambayo Adui Zetu Huziogopa. Tumeshinda Kwa Wewe BWANA Na Tutashinda Tena Na Tena Kwa Wewe JEHOVAH BWANA, Jina Lako Libarikiwe Milele. Ni Kwa YESU KRISTO Na Kwa Jina La YESU KRISTO Aliye Hai Milele timeomba.
Amen Amen''
Baada ya maombi naomba tujifunze neno hili.
Maombi kwa mkristo ni jambo la kudumu.
Maombi ni maisha.
Kuomba Maombi Katika ROHO MTAKATIFU Ni Muhimu Sana.
Waefeso 6:18 ''kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika ROHO, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;''
Ngoja nikupe ushuhuda huu mfupi.
Kuna Wakati Nilikuwa Na Mzigo Wa Kuwaombea Watu Fulani Wengi Ili MUNGU Awasaidie, Walinisihi Sana Niwaombee Na Rohoni Niliambiwa Kuwaombea.
Jambo Hilo Halikuwa La Siku Moja, Na Niliomba Huku Na Mimi Nikiwa Katika Wakati Mgumu Sana Maana Huduma Yangu Mtandaoni Ilikuwa Inapigwa Vita Kuliko Kawaida Pia Kwenye Ulimwengu Wa Roho Niliona Mashambulizi Makubwa Dhidi Yangu Kwa Sababu Ya Neno La MUNGU.
Nilitamani Kuombea Huduma Yangu Hiyo Lakini Rohoni Niliona Tu Agizo La Kuwaombea Wale Ndugu Waliokuwa Kwenye Matatizo Makubwa Sana Wakati Huo.
Nilichojifunza Ni Hiki Kwenye Maombi Fuata Maamuzi Ya ROHO MTAKATIFU Maana Wakati Mimi Nawaombea Wale Ndugu Kuna Mama Mmoja Mwanza Aliona Hatari Iliyokuwa Inanikabili Aliagizwa Na ROHO Kufunga Siku 5 Ili Kuniombea. Hapa Unaona Umuhimu Wa ROHO Kwenye Maombi Maana Nilipokuwa Nawabebea Mzigo Wengine Ndipo Na Mimi Nilibebewa Zaidi Mizigo Yangu.
Ndugu Zangu Ombea Unalosukumwa Kuliombea Maana Hilo Ndilo Muhimu sana Kwako Kwa Wakati Huo.
Inawezekana kabisa umefunga ili uombee kupata mchumba lakini ulipoanza tu kuomba ukawa unasikia msukumo wa kumuombea tu mtumishi fulani wa MUNGU, ambaye hata humjui na hata kama unamujua lakini hujui kama yuko katika wakati mgumu. lakini kwa MUNGU hakuna kazi ya hasara.
inawezekana kabisa kitendo cha wewe kumuombea mtumishi wa MUNGU ndio kinatoa jibu la hitaji lako. Mtumishi yule wa MUNGU baada ya kuvuka katika jaribu alilokuwa nalo kwa sababu ya maombi yako yaliyomvusha iko siku ROHO wa MUNGU ambaye ni yeye yule kwako na kwa mtumishi yule anaweza akamtumia mtumishi yule kukutabiria jambo la baraka yako ya ndoa ambayo hata kama wangekupinga wachawi 60 bado utashinda maana ROHO wa MUNGU yuko kazini.
1 Kor 12:6-11 ''Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali MUNGU ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa ROHO kwa kufaidiana. Maana mtu mmoja kwa ROHO apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo ROHO yeye yule; mwingine imani katika ROHO yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika ROHO yule mmoja; na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; lakini kazi hizi zote huzitenda ROHO huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.''
Ni muhimu sana kuongozwa na ROHO MTAKATIFU maana yeye anaweza kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja.
Katika maombi pia ni muhimu sana kuomba katika ROHO maana kile ROHO atakuambia uombee ndicho muhimu zaidi kwako kwa wakati huo.
Wako watu walikuwa wana mahitaji yao mazuri tu lakini walipoanza kuomba ROHO alisema nao kwamba wawaombee watu fulani ambao ni maadui zao, ni ngumu wewe mwenye adui zako harafu uambiwe uombee adui zako, kibinadamu ni kama haina faida lakini jambo hilo ndilo muhimu zaidi kwako kuliombea kwa wakati huo maana ROHO wa MUNGU analiona jambo mwisho kabla ya mwanzo. Inawezekana wewe hupokei kwa sababu ya chuki uliyonayo moyoni mwako dhidi ya watu fulani lakini kwa kuambiwa uwaombee hao unaowachukia itakufanya uweze kuwasamehe kisha ndipo utapokea baraka yako unayoiombea kila siku.
Kwa Mkristo aliyeokoka ni lazima aenende kwa ROHO, Ni lazima amtii ROHO wa MUNGU siku zote na Biblia inasema hivi
'' Tukiishi kwa ROHO, na tuenende kwa ROHO.-Wagalatia 5:25''
Jambo la kujua ni hili;
=Alipo MUNGU Na YESU Yuko Hapo Hapo.
=Alipo YESU Na ROHO MTAKATIFU Yuko Hapo Hapo
= Alipo ROHO MTAKATIFU Na Damu Ya YESU Ipo Hapo Hapo.
=Alipo MUNGU BABA Na MUNGU MWANA pia ROHO MTAKATIFU Wapo Hapo Hapo.
Ni muhimu sana pia kuijua hii tahadhari inayotolewa na Biblia kwamba ''Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya ROHO wa MUNGU; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. -1 Kor 2:14 ''
Je, wewe ni mwanadamu wa tabia ya mwili au rohoni?
Mwanadamu wa tabia ya mwilini hawezi kupokea maagizo ya ROHO MTAKATIFU wala hawezi kuyaelewa wakati mwingine maana maagizo ya ROHO wa MUNGU hutambulikana kwa jinsi ya Rohoni na sio mwilini.
Tamani kuomba katika ROHO MTAKATIFU.
Omba ROHO akujaze ufahamu wa kiMUNGU na akujaze nguvu zake.
Hakikisha unakuwa mtu wa Rohoni na sio mwilini maana mambo ya MUNGU ambayo unayahitaji hupatikana Rohoni na sio mwilini.
Kama wewe ni mtu wa mwilini kisha unataka baraka za rohoni basi itakusumbua sana maana inabidi uwe mtu wa rohoni ndipo utapokea vya rohoni.
1 Kor 2:11 '' Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya MUNGU hakuna ayafahamuye ila ROHO wa MUNGU.''
=Mambo ya MUNGU ayafahamuye ila ROHO wa MUNGU.
Kwa maneno mengine ina maana ya kuwa, ikiwa tunahitaji kuyafahamu mambo ya MUNGU inatubidi tujifunze kushirikiana na ROHO MTAKATIFU.
Naamini hakika kuanzia sasa utakuwa mtu wa rohoni na sio mtu wa mwilini.
Mtu wa rohoni ni mwana maombi na hujiunga na kundi la maombi kanisani.
Mtu wa rohoni hujifunza Neno la MUNGU na kuliishi.
Mtu wa rohoni ni mwaminifu kwa MUNGU.
Mtu wa Rohoni maisha yake amemkabidhi BWANA YESU na anatembea katika utakatifu wa kweli.
' Tukiishi kwa ROHO, na tuenende kwa ROHO.-Wagalatia 5:25''
Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
KWANINI WEWE HUSHUHUDII WENGINE ILI WAJE KWA YESU?
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze neno la Muhimu sana.
Moja ya kazi muhimu ambayo kila mkristo amepewa na MUNGU ni kushuhudia kwa wengine habari njema za ufalme wa MUNGU.
Biblia inawaita wakristo waliookoka kwamba jina lao ni ''Watangaza fadhili za BWANA''
Zaburi 103:17 ''Bali fadhili za BWANA zina wamchao Tangu milele hata milele, Na haki yake ina wana wa wana;''
=Una neema wewe maana umempokea BWANA YESU na hakika umeokoka, lakini kuokoka kwako kuna maana kwamba uepukane na dhambi na pia kuokoka kwako ni ili uwasaidie na ndugu zako kuokoka. Ndio maana Biblia inakuita wewe ni mtangaza fadhili za BWANA YESU.
Biblia haikuishia hapo bali inasema ''Mwimbieni BWANA, libarikini jina lake, Tangazeni wokovu wake siku kwa siku. Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake. Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana. Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote. Maana miungu yote ya watu si kitu, Lakini BWANA ndiye aliyezifanya mbingu. Heshima na adhama ziko mbele zake, Nguvu na uzuri zimo katika patakatifu pake. Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu, Mpeni BWANA utukufu na nguvu. Mpeni BWANA utukufu wa jina lake, Leteni sadaka mkaziingie nyua zake. Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu, Tetemekeni mbele zake, nchi yote. -Zaburi 96:2-9''
=Inawezekana kabisa ndugu hujui jambo hili lakini naomba ujue kwamba BWANA YESU amekupa jukumu la wewe kuwa shahidi wake kwa watu wengine.
Mathayo 28:19-20 ''Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la BABA, na MWANA, na ROHO MTAKATIFU; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.''
=Inawezekana kabisa hujui uanzie wapi kushuhudia.
=Inawezekana kabisa unawaza labda kama ukipata neema ya kwenda chuo cha Biblia ndipo utaanza kushuhudia wengine habari za ufalme wa MUNGU. Lakini ulishawahi kujiuliza swali hili kwamba ''Kama kila siku watu wanakufa, je hadi umalize chuo ndipo ushuhudie, je watakuwa wamekufa watu wangapi ambao ulitakiwa wewe uwashuhudie kabla hawajafariki?''
Jibu ni wengi sana. Lakini BWANA YESU anatuambia mimi na wewe leo kwamba
'' Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.-Marko 16:15''
MUNGU mwenyewe ndiye aliyeanza kushuhudia na akatupa kielelezo sisi wateule wake.
MUNGU aliandaa njia ya wokovu moja tu kwa wanadamu wote na njia hiyo ni YESU KRISTO pekee hivyo MUNGU mwenyewe akawa wa kwanza kushuhudia njia ya wokovu aliyoiandaa mwenyewe.
1 Yohana 5:9b ''Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa MUNGU ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa MUNGU ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe.''
Dada mmoja aliyekuwa mgonjwa sana kule Zanzibar alishuhudiwa kila siku kwamba aokoke na BWANA YESU atampa uzima wa milele, Dada yule alikuwa katika kukubali kuokoka lakini ndugu zake wakamkemea na kumshauri kwamba asikubali kuwa mkristo. Yule dada aliwasikiliza ndugu zake na jioni moja vijana wenzangu ambao tulikuwa tunashuhudia pamoja walimtembelea na kumwambia habari za kuokoka, akakataa na kuanza kumsanifu BWANA YESU. Kwa sababu ziku zake za kuishi zilikuwa mwishoni kabisa na alikuwa mgonjwa mahututi hivyo aliikataa neema ya KRISTO maana BWANA YESU alitaka kumwokoa hata katika mazingira yale, Dada alikataa lakini baada ya hapo haikupitia hata wiki moja yule dada akafariki lakini wakati anafariki alianza kulia kwa nguvu sana huku akimtaja BWANA YESU, Yule Dada katika mazingira ya roho yake kuachana na Mwili ni kama alimuona BWANA YESU maana alianza kulia na kumwita YESU amsaidie, aliona anakoelekea siku hivyo alimhitaji BWANA YESU maana hapo ndipo alipojua kwamba nje na KRISTO YESU hakuna uzima wa milele. alikufa akiita YESUUUUUUUUUUUUU.
Mimi na wewe hatuwezi kujua baada ya hapo lakini napenda kukuambia kwamba kama Watu tuliookoka tunalo jukumu Kubwa sana la kuwashirikisha wengine upendo wa MUNGU wa wokovu.
Inawezekana kabisa hujui utaanzaje kushuhudia lakini lakini mimi najua ukiamua unaweza sana hata kama umeokoka jana tu.
Ngoja nikupe ushuhuda huu mwingine.
Kwa muda wa miaka mitatu na nusu sasa nimeandika masomo mtandaoni zaidi ya 400, Katika masomo hayo sikuacha hata siku moja kumwambia mtu kwamba anatakiwa aokoke. Kijana mmoja ambaye ni Mkristo anaishi mkoa wa mbali sana kutoka hapa Dar es salamm alijiona hawezi kushuhudiwa wengine japokua alitamani sana kushuhudia, na ndani yake kulikuwa na agazo la kuwashuhudia wengine. Alichokifanya kijana yule ni kuingia katika blog yangu na Ku-copy baadhi ya masomo yangu Kisha kuya-Print Kwenye karatasi nyingi na kuingia mitaani kuwagawia watu aliokutana nao bila kuwaeleza mambo mengi maana alijiona hajui, Kwa njia hiyo aliwashuhudiwa wengi na hadi anakuja kunipa ushuhuda huo alikuwa amewashuhudia watu wengi sana.
Hiyo ni njia mojawapo tu ya kushuhudia, yeye alitumia gharama kidogo lakini ujumbe niliokuwa nimeuandika ndio ulioshuhudia maana ulikuwa ni ujumbe mkali wa kuonya na kuwataka watu waokoke.
Ndugu yangu kama huyo kijana alitumia ujumbe wangu kushuhudia na akapata kondoo wengi je mfano kwa njia hiyo tu ya yule ndugu kama watu 500 wakifanya hivyo itakuwaje? maana mitandaoni kuna masomo mengi sana ya watumishi mbalimbali wa kweli wanaofundisha Wokovu kila siku hivyo kama watu watakuwa wanatumia jumbe hizo kuwasaidia na wengine unadhani injili haitawafikia watu wengi zaidi?
Kwa MUNGU hakuna kazi ya hasara, wewe ukishuhudia haijalishi umetumia ujumbe wa nani lakini Thawabu yako iko mbinguni na MUNGU atakulipa. Wewe utakuwa mtu mwenye faida zaidi katika ufalme wa MUNGU.
Wewe utakuwa mtumishi wa MUNGU.
Kuna njia nyingi sana za kushuhudia hata kama hujui uanzeje.
=Mfano kama kuna mkutano wa injili mahali fulani na wewe ukamwalika mtu mmoja mwende naye kwenye mkutano huo na yeye akaenda akalipokea Neno la MUNGU basi hakika hapo umeshuhudia.
=Kama kuna kipindi fulani kwenye redio ambako injili halisi inahubiriwa kisha wewe ukamwalika mtu kusikiliza kipindi hicho cha mahubiri, hakika hapo umeshuhudia.
=Kama wewe utajiwekea malengo kwamba kila mwaka lazima uhakikishe unapeleka watu 5 kanisani hakika utaweza maana MUNGU atasimamia maono yako hayo kwa utukufu wake.
Kila Mteule wa BWANA YESU anatakiwa ashuhudie injili kwa watu wengine.
1 Petro 4:10-11 ''kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za MUNGU. Mtu akisema, na aseme kama mausia ya MUNGU; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na MUNGU; ili MUNGU atukuzwe katika mambo yote kwa YESU KRISTO. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.''
=Hata kama utashuhudia harafu hakuna aliyeokoka wewe usijali maana hapo umepanda mbegu na mbegu yako hiyo ipo siku itaota tu.
Wewe ni Wakili wa BWANA YESU maana yake unamwakilisha BWANA YESU katika kuwakusanya kondoo wake, fanya kazi hiyo ya uwakili kwa uaminifu na utapewa taji mbinguni.
1 Kor 4:1-2 ''Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa KRISTO, na mawakili wa siri za MUNGU. Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.''
Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
HARIBU MADHABAHU YA POMBE KATIKA UKOO WAKO.
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze neno la MUNGU.
Warumi 13:13-14 '' Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu. Bali mvaeni BWANA YESU KRISTO, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake.''
-Watu wote tunatakiwa twenende kwa adabu; Sio kwa ulafi na ulevi, sio kwa ufisadi wala uasherati.
Mengi yamesemwa katika andiko hapo juu lakini mimi leo nazungumzia pombe.
Pombe ni pando la adui ili kuhakikisha watu hawafiki uzima wa milele.
Pombe ni madhabahu ya shetani ambayo inauwezo wa kuiteka familia nzima au ukoo mzima.
Madhabahu hii ni hatari na kama ikiwakamata ukoo mzima mtajikuta mnaabudu tu katika madhehebu ambayo wanaruhusu pombe maana hata wao wanamilikiwa na madhabahu hiyo ya pombe. yaani hata leo unaweza ukafanya utafiti kwamba kuna baadhi ya koo utakuta ukoo mzima wanasali dhehebu fulani sio kwa sababu ni zuri ila ni kwa sababu hawawezi kuacha pombe ndio maana wako katika dhehebu hilo. Lakini katika Biblia sehemu nyingi tu imesema kwamba hakuna mbinguni ya mlevi hata mmoja.
Kama mlevi anataka mbingu basi aokoke na atubu kisha aanze kuishi maisha mataktifu na aache dhambi zake ikiwepo pombe anatakiwa aiache maana haina faida kwake hata moja bali pombe imejaa hasara tu.
Waefeso 5:18 ''Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;''.
Biblia haikuishia hapo tu kukataza pombe au mvinyo kwa lugha nyingine bali hapa tena Biblia inasema hivi
''Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.-1 Kor 6:9-10 ''
=Katika maandiko haya hapo juu walevi wanaitwa wadhalimu na imesemwa hapo kwamba wathalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU.
Walevi hawako katika msafara wa waenda mbinguni ndivyo Biblia imesema. sasa mafundisho ya kuruhusu pombe yanatoka wapi? Wakati Biblia imesema hakuna mbinguni ya walevi?
Ni matokeo ya madhabahu ya pombe kutawala hadi kwa baadhi ya viongozi wa kanisa ndio maana wanafundisha watu wanywe pombe, jambo ambalo halifai kufundishwa na mtumishi wa MUNGU aliye hai.
Pombe haina faida hata moja lakini ina madhara zaidi ya kumi.
Hebu ona katika andiko andiko hili ili uone jinsi pombe inavyoweza kumfanya mtu kuwa mtumwa.
Mithali 23:29-35 '' Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu?
Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika. Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu; Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira. Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka. Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti. Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.''
-Kupitia maandiko hayo tu unaweza ukaona madhara zaidi ya 10 ya pombe.
Ni muhimu sana ndugu yangu kujitenga na pombe na ni muhimu sana kuomba maombi ya kuikomboa familia yako ili iepukane na ulevi.
-Unakuta katika ukoo kijana anataka kujinasua ili aache ulevi ambao umeleta umasikini kwake na kwa ukoo mzima lakini hawezi.
-Inawezekana kabisa dada umeolewa katika ukoo ambao unamilikiwa na madhabahuu ni ya kipepo na mme wako mwanzo hakuwa mlevi lakini miaka 2 baada ya ndoa anaanza tena kunywa maana ndio ukoo wao ulivyo, unamilikiwa na madhabahu ya pombe. unaweza ukamchukia mume wako kumbe madhabahu inayomtumikisha ndio inatakiwa kuharibiwa.
Haribu madhabahu ya pombe katika ukoo wenu.
-Unakuta mama analia kila siku maana wakilima shamba miezi 6 kisha wanavuma mazao , baba wa familia akienda tu kuuza mazao hayo anarudi baada ya siku 4 huku hana hata Shilingi mia. unajiuliza pesa hiyo familia imeitafuta kwa miezi 6 au zaidi lakini inakuja kutumiwa na baba wa familia tu kwa siku 4 kwa sababu ya pombe.
-Ndugu uliyeokoka hakikisha unaukomboa ukoo wako kwa maombi.
-Wewe ambaye umepata neema ya Wokovu wa BWANA YESU hakikisha unaomba ili ukoo wako wawe huru mbali na jini pombe linalowatesa.
BWANA YESU awape neema ya wokovu wake ndugu zako na familia yako.
Habakuki 2:15-16 '' Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!Umejaa aibu badala ya utukufu; unywe nawe, uwe kama mtu asiyetahiriwa; kikombe cha mkono wa kuume wa BWANA kitageuzwa ukipokee, na aibu kuu itakuwa juu ya utukufu wako. ''
Ndugu zangu nawasihini licha ya kuacha vileo unapaswa pia kutompa kileo mtu yeyote yule. haijalishi ni baba, ni mama au ni nani? Kwa kufanya hivyo unashiriki dhambi isiyo ya Kwako, kumbuka dhambi zote ni sawa na hukumu yake inajulikana.
Wewe ndugu uanyefanya dhambi ikiwepo ya ulevi naomba ujue kwamba;
Kujifurahisha katika dhambi kwa muda kidogo kisha ukaingia kwenye ziwa la moto haitakusaidia chochote.
Muda wa kugeuka ni leo, BWANA YESU anakungoja umpokee leo. najua una marafiki wengi wanaokushawishi katika mabaya lakini naomba ujue kwamba siku BWANA YESU akirudi utasimama peke yako kwenye hukumu, rafiki anayekuchochea leo ili umfuate siku hiyo hatakuwa msaada kwako hata mmoja.
Neno hili naomba liwe lako leo na umpokee YESU.
MUNGU BABA akupe macho ya kuona na kuelewa jambo hili nilisemalo leo.
Isaya 5:11 ''Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao! ''
Mambo ya dunia mengi yamewafanya wanadamu wamsahau MUNGU.
Kazi zimewafanya wanadamu wengi kumsahau MUNGU.
Japokuwa hakuna mwanadamu hata mmoja ambaye siku ya mwisho atajitetea Kwa ajili ya kazi yake serikalini au kwenye kampuni.
Kazi ya mtu ya sasa haitakuwa na msaada siku ile.
Sio kwamba kazi ni mbaya lakini kitendo cha kuthamini kazi zaidi ya MUNGU wako ambaye ndiye aliyekubariki hiyo kazi ni vibaya.
Na wengi wenu licha ya kuwa busy na kazi lakini mkitoka kazini hamwendi kanisani bali mnaenda bar kunywa pombe na kufanya starehe zingine.
Kila mtu ukimwambia aende kanisani atakuambia kazi imembana hivyo yuko busy lakini mtu huyo huyo hata siku moja hajawahi kukosa bar kwenye pombe.
Ndugu Ambaye umeokoka nakusihi sana kuomba sana kwa ajili ya familia yako na ukoo wako ili BWANA YESU awanasue kutoka kwenye dhambi ikiwepo pombe.
Usifurahie ndugu zako wakose muda wa kwenda kanisani lakini muda wa kwenda vilabuni wanao.
Ukitibu pepo pombe hakika utakuwa umepunguza mengi mabaya katika ukoo wako.
Chanzo kikuuu cha watu kufa na ukimwi wakati mwingine ni pombe maana baada ya kulewa ufahamu unaondoka na mtu huyu anaweza akafanya lolote au akafanyiwa lolote.
2 Kor 6:16-18 '' Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la MUNGU na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la MUNGU aliye hai; kama MUNGU alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa MUNGU wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema BWANA, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa BABA kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, ''
Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
Subscribe to:
Posts (Atom)