![]() |
Na Mchungaji Issaya. |
BWANA YESU ASIFIWE !
Unaweza kuteseka sana hata kama umeokoka kwakutojua nguvu iliyoko ndani ya jina la Yesu inavyo weza kukusaidia
Mungu anasema katika Zekaria 10 :12 : ‘Nami nitawatia nguvu katika BWANA,nao watatembea huku na huko katika Jina lake asema BWANA’
Ndugu mtu wa Mungu,Napenda kwanza ufahamu kwamba Jina la YESU lilikuwa Jina la Mungu wetu akamrithisha YESU,
najua unashangaa ila embu soma Ebrania 1 :4 :’Amefanyika bora kupita malaika,kwa kadiri ya Jina alilorithi lilivyo tukufu kuliko lao.’Kwa hiyo huo mstari wa Zekaria 10 :12 Mungu anasema kuwa atatutia nguvu katika Jina la YESU.
JINA LIPITALO MAJINA YOTE :
Ndugu katika Kristo,Jina la YESU ni Jina linalopita majina yote hapa duniani,kule mbinguni(Ebrania 1 :4) na hata kule kuzimu.Kama Biblia inavyosema Wafilipi 2 :9 : ‘Mungu alimwadhimisha mno,akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina’
Jina la YESU linaokoa,linatubariki,linatuunganisha na Mungu n.k.
NGUVU ILIYOMO KWENYE JINA LA YESU:
NGUVU YA KUFANYA YOTE.
Ndugu,ukweli ni kwamba Jina la YESU linayo nguvu ya kumsaidia kila mtu kufanya kila jambo analotaka kulifanya hapa duniani,mradi tuu iwe ni jambo jema la kumpendeza Mungu.Iwe ni kusoma,kuhubiri kuimba au lolote lile. Angalia Neno la Mungu linavyosema katika Wakolosai 3 :17 : ‘Kila mfanyalo kwa neno au kwa tendo,fanyeni yote kwa Jina la YESU
NGUVU YA KUHUBIRI INJILI YA MUNGU.
Watumishi wote wa Mungu wanapaswa kufahamu kuwa Jina la YESU lina nguvu ambayo itatuwezesha kwenda huku na huko katika kutangaza Injili ya Mungu wetu,kwa maana ni lazima tumuombe Mungu ili atupe nguvu zake.Kumbuka mstari tuliousoma hapo juu wa Zekaria 10 :12.
NGUVU YA KUTULINDA SISI SOTE.
Jina la YESU pia lina nguvu za ajabu sana,na linaweza kabisa kutulinda dhidi ya mapepo,wachawi,majambazi,wezi,ajali na kila hatari iliyopo hapa duniani.Angalia pia Biblia inachosema katika kitabu cha Yohana 17 :11 : ‘.......uwalinde kwa NGUVU YA JINA L AKO ULILONIPA(Jina la YESU).Hayo ni maombi ya YESU akiwaombea wanafunzi wake kwa Mungu,anamwomba awalinde kwa nguvu iliyo kwenye jina la YESU.Tunachotakiwa ni kumwomba Mungu atulinde kwa nguvu iliyo kwenye jina la YESU.
UPONYAJI NA UKOMBOZI
Bwana YESU alisema ‘Kwa kutumia Jina langu watatoa pepo,watasema kwa lugha mpya,watashika nyoka,hata wakinywa kitu cha kufisha hakitawadhuru kabisa,wataweka mikono yao juu ya wagonjwa nao watapata afya’Ndugu napenda ufahamu kuwa Jina la YESU lina nguvu inayotuwezesha kumtumikia Mungu kwa kulitumia jina hilo na kazi ya Mungu ikafanyika.Ni muhimu basi kuomba nguvu ya Jina la YESU kabla ya kwenda kuombea wagonjwa au kukemea pepo au kufanya huduma ya ukombozi au huduma yoyote ile.
LINAMLETA YESU PALE TULIPO.
YESU mwenyewe alisema katika Matayo 18 :20 : ‘Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa Jina langu,nami nipo papo hapo katikati yao’Hii ina maana kuwa popote pale tunapokusanyika halafu tukalitaja Jina la YESU,yeye mwenyewe YESU anashuka na kuwa pamoja nasi hata kama hatumwoni kwa macho yetu.Basi hii ni nguvu nyingine ambayo Mungu ameiweka kwenye Jina la YESU.
NGUVU ZA KIVITA :
Watu wengi hawategemei kuwa Jina la YESU lina nguvu ya kutusaidia katika vita tulivyonavyo hapa duniani.Ni rahisi kwao kuamini kuwa Jina hili lina nguvu kutushindia vita vya kiroho lakini si vya majeshi ya wanadamu.Kama umeingia vitani kwa kibali cha Mungu,basi Jina la YESU lina uwezo wa kukusaidia ushinde hivyo vita.Mkumbuke Mfalme Daudi wakati alipomwua Goliathi kwa kombeo la jiwe,hebu tusome Biblia 1Samweli 17 :45 : ‘Daudi akamwambia....lakini mimi nakujia kwa Jina la BWANA(Jina la YESU) wa majeshi,Mungu wa majeshi ya Israeli..’Ni wazi kuwa yule Goliathi alikuwa amejiandaa kuingia vitani hii ikiwa ni pamoja na kuvaa mavazi ya kuulinda mwili wake,na kwasababu hiyo ilikuwa si rahisi kwa nguvu za kibinadamu kumuua Golithi kwa jiwe la kombeo,lakini yeye Daudi hakuingia vitani kwa nguvu zake bali aliingia kwa nguvu za Jina la YESU,alipoingia vitani kwa Jina hilo,YESU aliteremsha msaada na nguvu zake kwa Daudi ndio maana akamwua Goliathi kwa jiwe la kombeo.Soma pia Zaburi 44 :5b,na Zaburi 20 :7 : ‘Hawa wanataja magari,hawa farasi lakini mimi nitalitaja Jina la Bwana Mungu wangu(Jina la YESU)’
KUAMURU UNACHOTAKA KITOKEE KUTOKEA.
Kwa kutumia jina la YESU tunaweza kuamuru chochote ambacho ni chema mbele za Mungu kitokee kikatokea kweli.
ITUMIE HIYO NGUVU
Natumaini kuwa umejifunza na kufahamu baadhi ya nguvu zilizomo kwenye Jina hili la ajabu,Jina la YESU Kristo.Sasa unachotakiwa kufanya ni wewe kuitumia hiyo nguvu iliyopo kwenye Jina hilo.
Ili uweze kulitumia Jina la YESU ni muhimu kumuomba Mungu mambo yafuatayo :
UHALALI WA KULITUMIA :
Ili kulitumia Jina la YESU ni lazima Mungu akupe uhalali wa kulitumia Jina hilo.Kumbuka kilichowapata watoto wa mtu mmoja aliyeitwa Skewa(Matendo 18 :11-16),vijana hawa walitaka kulitumia Jina la YESU kukemea pepo huku hawajaokoka,matokeo yake yule pepo akawadhuru.Kupata uhalaliwa Kulitumia Jina la YESU ni lazima KUOKOKA kwanza kama hujaokoka.
IMANI JUU YA JINA HILO :
Ili kulitumia Jina la YESU ni lazima kwanza uwe na imani juu ya Jina hilo,uliamini kuwa linaweza YOTE.Kama Biblia isemavyo kuwa kuwa Imani huja kwa kusikia Neno la Kristo(Warumi 10 :17)basi ni lazima kusoma maandiko sahihi yanayofundisha kuhusu Jina la YESU.
MAMLAKA YA KULITUMIA :
Ukishaokoka unakuwa na uhalali wa kulitumia Jina la YESU lakini si mamlaka,hivyo ni lazima kumwomba Mungu akupe mamlaka ya kulitumia Jina hilo.
UPAKO WA KULITUMIA :
Unahitaji pia upako kutoka kwa Mungu wa kukusaidia na kukufundisha kulitumia Jina la YESU katika maisha yako,mwombe Mungu akupe upako huo.
MBINU ZA KULITUMIA :
Huwezi kulitumia Jina la YESU bila kujua mbinu za kulitumia,hivyo mwombe Mungu akupe mbinu za kulitumia Jina hilo,naye atakufundisha.
Natumaini kuwa somo hilo limekusaidia sana,tafadhali nifahamishe namna somo hili lilivyokusaidia.
Emen
ReplyDeleteMungu akubariki baba kwa ufunuo hui kujuwa jinsi ya kutumia Jina la yesu
ReplyDeleteAmen sana
ReplyDeleteNimeongeza sana ufahamu wa jina la yesu kristo
ReplyDelete